About DDD

DIGITAL DIVIDE DATA (DDD)

DDD hutoa huduma ya maudhui ya kidigitali na ufumbuzi wa utafiti duniani kote . Wateja wetu hupokea huduma zenye kiwango cha hali ya juu zinazolingana na huduma zetu za maudhui ya kidigitali. Kwa wakati huohuo, DDD ina changamoto ya kijamii ambayo inawezesha vijana kutoka familia zisizojiweza kupata nafasi za kitaaluma zianazowawezesha kupata kipato cha juu. Muundo huu uliowekwa na DDD mwaka 2001, ambao kwa sasa tunaiuita “ajira kwa watu wenye hali ya chini ya kimaisha kutumia mtandao”, umekua ukitumika na makampuni mengi duniani kote.

Suluhisho la DDD kwenye maudhui ya kidigitali ni yafuatayo:

Wateja wa DDD ni kama, kawachapishaji wakubwa, vyombo vya habari na taasisi nyinginezo zinahusika na habari; watumiaji na wanunuzi wadogowadogo; wakala wa serikali; makataba; makumbusho na nyaraka za kumbukumbu; uwekezaji, mawasiliano ya simu na makampuni ya uzalishaji na makampuni ya kibinafsi.

Tangu 2001 , mpango wa DDD umeongeza kipato cha vijana Kambodia,Laosi na Kenya kwa asilimia zaidi ya dolla za kimarekani 250,000,000. Muundo wa kijamii wa DDD ni wa kipekee kwasababu vijana wana nafasi ya kuhitimu elimu yao ya juu huku wakipata uzoefu wa kazi.

DDD imekua ikitambulika duniani kote kwa huduma bora, ubunifu na uwajibikaji wa kijamii. DDD imepokea tuzo nyingi na kutambulika katika nyazfa tofauti za kijamii, Baraza la Global Sourcing iliwatunukia DDD tuzo la 3S kwa ajili ya uwajibikaji endelevu kwa jamii. DDD ipo maradufu katika orodha ya makampuni ya 100 bora binafsi duniani kama ilivyoandikwa na waandishi wa jarida la Global na pia DDD imepokea tuzo kutoka Google ya ubunifu katika biashara ya kugawa kazi.